◉WhatsApp
⌖Makole, Dodoma

MAFUNZO KWA AJILI YA HUDUMA

Aenon Faith Bible College (AFBC) – Dodoma Campus

Elimu ya Biblia yenye msingi wa imani ya Kipentekoste kwa wachungaji, watumishi na viongozi wa Kanisa.

KUHUSU CHUO

Aenon Faith Bible College (AFBC) – Dodoma Campus

Aenon Faith Bible College (AFBC), Dodoma Campus ni taasisi ya elimu ya Biblia inayolenga kuwaandaa wachungaji, watumishi na viongozi wa Kanisa kwa kuwapatia elimu ya Biblia yenye msingi wa imani ya Kipentekoste. Chuo kinaamini kwamba elimu ya Biblia ni msingi muhimu katika kumjenga mtumishi mwenye maarifa, uadilifu na uwezo wa kulitumikia Kanisa na jamii kwa ufanisi. AFBC ilianzishwa mwaka 2007 huko Mlali, na Kampasi ya Dodoma ilianzishwa Februari 2025.

ILIANZISHWA2007

Mlali


KAMPASI YA DODOMAFebruari 2025

DIRA NA DHAMIRA

Kujengwa katika Neno na Kutumwa Kuhudumu

DIRA

Msingi imara katika Neno

Kuwa chuo kinachoandaa watumishi wa Mungu wenye msingi imara katika Neno la Mungu, tabia njema na uwezo wa ki-Mungu wa kubadilisha jamii.

DHAMIRA

Elimu kwa ajili ya shamba la Bwana

Kuwa na watumishi wenye elimu ya Biblia na kuitumia ipasavyo shambani mwa Bwana.

PROGRAMU YA ELIMU

Diploma ya Thiolojia

Diploma ya Thiolojia. Masomo ya ziada yanajumuisha maarifa kwa ujumla na kozi ya awali ya lugha ya Kiingereza.

MFUMO WA MASOMO

Mihula 3 kwa mwaka

Chuo kina mihula mitatu (3) kwa mwaka. Kila muhula una wiki 10 za masomo, na kwa wastani mwanafunzi hufundishwa masomo 8 katika kila muhula. Udahili wa wanafunzi hufanyika mwezi Februari kila mwaka.

MSINGI WA CHUO

Elimu ya Biblia yenye mwelekeo wa Kipentekoste

Aenon Faith Bible College inasimama katika msingi wa elimu ya Biblia yenye mwelekeo wa Kipentekoste, ikiwa na lengo la kuwaandaa watumishi watakaoweza kulitafsiri na kulitumia Neno la Mungu kwa usahihi katika mazingira halisi ya huduma.

“Kuwa Mtumishi Bora Inawezekana.”KAULI MBIU YA CHUO

USAJILI

Taratibu za Kitaifa

Kwa sasa, taratibu za usajili wa Aenon Faith Bible College zinaendelea katika ngazi ya PHAMT Taifa. Mfumo wa usajili unatarajiwa kuwa wa kitaifa, ambapo vyuo vitafanya kazi kama matawi ya taasisi hiyo.

UDAHILI NA MAWASILIANO

Jiunge na AFBC Dodoma Campus

Udahili wa wanafunzi hufanyika mwezi Februari kila mwaka. Wasiliana na chuo kwa maelezo ya vigezo, ada na utaratibu wa kuomba.

Wasiliana Nasi